Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu yasaidia pande hasimu za Sudan kuwaachilia wafungwa 565
2024-02-27 10:53:31| cri

Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu tarehe 26 ilitangaza kwamba tangu kuzuka kwa mgogoro wa kijeshi nchini Sudan mwaka jana, shirika hilo lisiloegemea upande wowote, limesaidia pande zote mbili za mgogoro kuachilia watu 565 walioshikiliwa, wakiwemo watoto 91 na wafuasi 170 waliojeruhiwa wa pande hizo mbili za mzozo.

Mgogoro wa kivita ulizuka tarehe 15 mwezi Aprili kati ya wanajeshi wa Sudan na vikosi vya msaada wa Haraka (RSF) katika mji mkuu Khartoum, ambao umeenea katika maeneo mengine na kuendelea hadi leo. Kwa mujibu wa ripoti kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, mgogoro huo umesababisha vifo vya takriban watu 13,900 na wengine takriban 27,700 kujeruhiwa.