Watu zaidi ya milioni 58 wakabiliwa na ukosefu wa chakula katika Pembe ya Afrika
2024-02-28 08:51:07| CRI

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Mamlaka ya maendeleo ya kiserikali ya Afrika Mashariki (IGAD) zimesema katika ripoti ya pamoja iliyotolewa Jumanne, kuwa takriban watu milioni 58.1 wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula kwenye Pembe ya Afrika.

FAO na IGAD zimesema kati ya watu hao, milioni 30.5 wanatoka nchi sita kati ya nne za wanachama wa IGAD Djibouti, Kenya, Somalia, Sudan Kusini na Uganda, na wengine milioni 27.6 wanatoka Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania.

Mashirika hayo yamesema kiwango cha juu cha ukosefu wa chakula kinaendelea katika sehemu mbalimbali ya kanda hiyo kutokana na mvua kubwa zinazoletwa na El Nino wakati wa msimu wa mvua kati ya mwezi Oktoba na Desemba mwaka 2023, haswa katika Pembe ya Afrika, pamoja na migogoro inayoendelea, uhamishaji wa makazi, na changamoto za uchumi wa jumla zilizodumu kwa muda mrefu.

Pia wamebainisha kuwa mbali na msukosuko wa chakula, Pembe ya Afrika pia inakabiliwa na milipuko mingi ya magonjwa ikiwemo kipindupindu, malaria, dengue na surua.