Maafisa wa UM watoa tahadhari kwamba eneo la kaskazini mwa Gaza litakumbwa na baa la njaa
2024-02-28 22:28:50| cri

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani Bw. Carl Skau jana alitahadharisha kwamba eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza litakabiliwa na baa la njaa, na kiwango cha utapiamlo kwa watoto huko Gaza kimekuwa kibaya zaidi duniani ambapo mtoto mmoja kati ya sita wenye umri wa chini ya miaka miwili wana tatizo la utapiamlo. Bw. Skau amesema kuwa wafanyakazi wa misaada hawawezi kutekeleza kazi ya utoaji wa msaada kwa kiwango kinachohitajika kama hakutakuwa na ruhusa ya ufikishaji wa msaada wa kibinadamu kwa usalama.

Licha ya hayo, mkurugenzi wa ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Ramesh Rajasingham pia amesema kuwa ifikapo mwishoni mwa Februari mwaka huu, watu wasiopungua laki 5.76 katika Ukanda wa Gaza watakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na njaa.