Maonesho ya Kukutana na Afrika 2024 yafunguliwa huko Johannesburg nchini Afrika Kusini
2024-02-28 09:00:51| criKukutana na Afrika, maonesho ya biashara barani Afrika yalifunguliwa jana huko Johannesburg nchini Afrika Kusini, ambapo kampuni 380 kutoka nchi 21 za Afrika zinaonesha bidhaa na huduma zao.

Waziri wa utalii wa Afrika Kusini Bi. Patricia de Lille amesema, hapo awali kampuni zilizoshiriki kwenye maonesho hayo nyingi zilikuwa kutoka Afrika Kusini, na nyingine chache zilikuwa kutoka sehemu nyingine za Afrika. Baada ya kupanua ushiriki kwa miaka mingi, hivi sasa maonesho hayo yamekuwa maonesho yanayoshirikisha nchi nyingi za Afrika.