Amadou Oury Bah ateuliwa kuwa waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Guinea
2024-02-28 10:29:46| cri

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya kienyeji, Rais wa mpito wa Guinea Kanali Mamady Doumbouya amemteua Amadou Oury Bah, mwenye umri wa miaka 65, kuwa waziri mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo. Tarehe 20 mwezi huu, rais Doumbouya alitangaza kuvunja serikali.