Mawaziri wa Afrika wakutana nchini Kenya na kujadili kuhimiza biashara ya umeme katika kanda yao
2024-02-28 08:52:01| CRI

Mawaziri wanaosimamia masuala ya umeme kutoka nchi za Afrika Mashariki wameanza mkutano wa siku tatu mjini Nairobi, kujadili namna ya kuhimiza biashara ya umeme katika kanda yao.

Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Afrika Mashariki kuhusu kuchangia umeme (EAPP) umewaleta pamoja maofisa wakuu wa serikali kutoka nchi 13 za Afrika ili kuendeleza ushirikiano wa kikanda katika sekta ya nishati.

Waziri wa nishati na petroli wa Kenya Bw. Davis Chirchir, amesema serikali katika kanda hiyo zimejitolea kupitisha sera, mipango na bajeti ambayo itasaidia kuongeza muunganisho wa gridi ya taifa ya umeme ya Afrika Mashariki.

Bw. Chirchir amesema tayari Kenya imevuna matunda ya ushirikiano wa kikanda kupitia mifumo ya nchi mbili ikiwa ni pamoja na kuagiza MW 200 za nishati mbadala kutoka kwa Ethiopia na kushiriki katika kubadilishana nishati na Uganda.