Watu 23 wafariki baada ya meli ya wahamiaji haramu kupinduka kaskazini mwa Senegal
2024-02-29 14:23:32| cri

Vyombo vya habari vya Senegal tarehe 28 Februari viliripoti kuwa meli moja iliyobeba wahamiaji haramu ilipinduka kwenye bahari ya kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo watu wasiopungua 23 wamekufa.

Shirika la habari la Senegal liliripoti kuwa meli hiyo ya wahamiaji haramu ilifunga safari yake kutoka mji wa Mbour, magharibi mwa Senegal, ikielekea Hispania. Hata hivyo ilipinduka tarehe 28 kwenye bahari ya kaskazini mwa Senegal, na kusimama karibu na mji wa bandari Saint-Louis nchini humo. Ripoti imenukuu habari kutoka idara ya zimamoto ya Senegal kuwa kuna watu takriban 280 ndani ya meli hiyo, waokoaji wamepata miili 23, na kazi ya uokoaji bado inaendelea.