Jumba la China laonesha bidhaa zake kwa mara ya kwanza kwenye Maonesho ya 60 ya Kilimo ya Kimataifa nchini Ufaransa
2024-02-29 14:28:36| cri

Katika Maonyesho ya 60 ya Kilimo ya Kimataifa nchini Ufaransa yaliyofanyika hivi karibuni, Jumba la China lilionesha bidhaa zake kwa mara ya kwanza.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964, Maonyesho ya Kilimo ya Kimataifa yamekuwa tukio kubwa zaidi la kilimo nchini Ufaransa. Maonyesho hayo yalivutia washiriki zaidi ya 1,100 kutoka nchi na kanda zaidi ya 30, na idadi ya wageni inatarajiwa kuwa zaidi ya 600,000.

Balozi wa China nchini Ufaransa Lu Shaye ametembelea maonyesho hayo, na kuwasiliana na wakuu wa maonyesho hayo, ambapo alisikiliza kuhusu maendeleo ya viwanda na ushirikiano mbalimbali na China.

Mkuu wa banda la China Xin Shaoying amesema kuwa hii ni hatua ya kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili katika muktadha wa maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Ufaransa. Ni jukwaa zuri hasa kwa mawasiliano baina ya watu wa nchi hizo mbili.

Katika maonyesho hayo wawakilishi wa Ufaransa wamesema China ni soko muhimu kwa bidhaa za kilimo na chakula za Ufaransa na wanatarajia kupanua ushirikiano na China ili kukuza zaidi bidhaa za kilimo na chakula za Ufaransa kuweza kuingia katika soko la China. Baadhi ya washiriki wa China pia wanatumai kupata bidhaa zenye ubora wa juu za Ufaransa.

Katika maonesho hayo Jumba la China lina eneo la mita za mraba zaidi ya 200, na karibu makampuni na taasisi 20 za China na Ufaransa zinashiriki kwa pamoja katika maonyesho hayo.