Uongozi wa CPC wajadili rasimu ya ripoti ya kazi ya serikali
2024-02-29 23:12:19| cri
Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ilikutana Alhamisi kujadili rasimu ya ripoti ya kazi ya serikali, ambayo itawasilishwa na Baraza la Serikali kwenye kikao cha mwaka cha Bunge la Umma la China katika mwezi huu wa Machi ili kujadiliwa. katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping aliongoza mkutano huo.
Kwenye mkutano huo ilibainishwa kuwa katika mwaka uliopita, licha ya mazingira magumu ya kimataifa na kazi ngumu za mageuzi, maendeleo na kudumisha utulivu, China imepita kwa wepesi kipindi cha kukabiliana na janga la UVIKO-19 na kushuhudia kuimarika kwa uchumi na ukuaji.
Kikao hicho kiliongeza kuwa, nchi imetimiza malengo makuu ya mwaka mzima katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ikipiga hatua thabiti katika kutafuta maendeleo yenye ubora wa juu na kujenga nchi ya kisasa ya ujamaa kwa pande zote.