Muhimbili kuanza kuhifadhi mbegu za uzazi
2024-02-29 11:13:35| cri

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua benki ya kuhifadhi mbegu za uzazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel akizungumza jana Februari 28, 2024 amesema Rais Samia atazindua benki hiyo hivi karibuni. Amesema MNH imeanza kuhifadhi mbegu hizo za uzazi na mtu akitaka kupata mtoto basi atafika hospitalini hapo na kupandikiziwa.

Amesema sio lazima watu waende nje kupandikiza kwani ndani ya hospitali hiyo wanapandikiza na kutunza mbegu hizo kwa muda wa miaka mitano hadi 10.