UNECA inaitaka Afrika kutumia mtaji wa asili ili kuharakisha mpito kwa uchumi wa kijani
2024-02-29 08:59:49| CRI

Naibu katibu mtendaji wa kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Bw. Antonio Pedro, amesema ni lazima Afrika itumie mtaji wake wa asili ili kuharakisha mabadiliko ya uchumi wa kijani.

Bw. Pedro amesema bara la Afrika likiwa linakabiliwa na mizigo na hatari nyingi kutokana na matukio na mifumo inayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi, linatakiwa kupitisha masuluhisho ya nyumbani kwa changamoto zake za maendeleo katika mfumo wa kifedha wa kimataifa.

Akiongea nchini Zimbabwe kwenye kikao cha 56 cha wiki moja cha UNECA cha Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi, Bw. Pedro amesema kuna fursa ya kipekee ya kubadilisha nchi za Afrika kikamilifu kuwa ni uchumi jumuishi, wenye utoaji mdogo wa hewa chafu na rasilimali zenye ufanisi.

Amesema hili linaweza kufikiwa kwa kuchanganya ahadi za mazingira na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ahadi za kijamii na kiuchumi na kutokomeza umaskini na kupunguza umaskini.