Vijiji vya katikati mwa Sudan vyashambuliwa kwa mara nyingi hivi karibuni
2024-02-29 14:22:57| cri

Habari kutoka vyombo vya habari vya Sudan zimesema kamati ya upinzani ambayo ni shirika la kijamii la Sudan ilitoa taarifa ikisema, vijiji vingi vilivyoko karibu na mji wa Hasaheisa, kaskazini mwa jimbo la Al Jazirah, katikati mwa Sudan vilishambuliwa kwa mara 39 na watu wenye silaha katika wiki tatu zilizopita, ambapo raia 46 wameuawa na watu 91 wamejeruhiwa. Ripoti hiyo imesema watu wenye silaha pia waliteketeza nyumba na kupora magari na mali.

Kamati hiyo ilishutumu kuwa watu wote waliofanya mashambulizi hayo wanatoka vikosi vya msaada wa haraka (RSF). Katika siku za karibuni, RSF iliwahi kujibu juu ya shutuma hizo likisema, kundi hilo halitakubali kamwe vurugu yoyote inayoharibu haki za raia. Litafanya uchunguzi juu ya tukio hilo na kuwawajibisha washambuliaji.