Msomi wa Tanzania: China ni rafiki wa kweli wa Afrika
2024-02-29 10:33:59| CRI

Karibu tena msikilizaji katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo, tutakuwa na ripoti inayohusu maandalizi ya mkutano wa FOCAC na pongezi zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha Sera ya Kimataifa-Afrika Bw. Omar Mjenga juu ya mchango muhimu wa FOCAC. Pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi na mmoja wa wanafunzi walioshirikiana kumwandikia rais Xi barua ya kumshukuru kwa hisani yake na kujibiwa kwa wakati.