Somalia yazindua mpango wa kuongeza juhudi za amani
2024-02-29 08:59:09| CRI

Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre amezindua mpango wa amani unaolenga kukuza mazungumzo na maridhiano kama sehemu ya juhudi za kuhimiza umoja nchini humo.

Bw. Abdi ambaye alizindua mpango huo uliopewa jina la “kanuni za Amani”, huko Mogadishu, amesisitiza dhamira thabiti ya serikali katika kuimarisha usalama na utulivu nchini humo.

Amesema chini ya utawala uliopo, hatua kubwa za kiusalama zimepatikana kuelekea kupatikana kwa amani ya kudumu nchini Somalia.

Amesema dunia ina wasiwasi kuhusu kuendelea kwa amani, hali inayofanya kuwa na umuhimu wa kupata sheria thabiti za kudhibiti kila mtu anayevuruga amani.

Bw. Abdi pia amebainisha kuwa Somalia iko kwenye njia ya amani, maendeleo na kufufua upya, akibainisha kuwa ni muhimu kuimarisha taasisi za serikali ili wananchi waweze kupata huduma wanazohitaji.