Kura za maoni za Marekani zaonyesha misimamo mikali ya kisiasa ni mojawapo ya wasiwasi mkubwa wa Wamarekani
2024-02-29 14:29:04| cri

Kura za maoni za hivi karibuni zilizotolewa na Reuters na Ipsos zilionyesha kuwa misimamo mikali ya kisiasa imeshinda uchumi na uhamiaji na kuwa moja ya maswala ambayo Wamarekani wanajali sana.

Kura za maoni za watu wazima 1,020 wa Marekani zilionyesha kuwa asilimia 21 ya wahojiwa walisema misimamo mikali ya kisiasa au vitisho kwa demokrasia ndio wasiwasi wao mkubwa, ikifuatiwa na masuala ya kiuchumi (yaliyochaguliwa na asilimia 19 ya wahojiwa) na masuala ya uhamiaji (yaliyochaguliwa na asilimia 18 ya wahojiwa).