Watu 23 wamekufa kwenye ajali ya kupinduka kwa boti ya wahamiaji katika pwani ya Senegal
2024-02-29 08:59:18| cri

Shirika la Habari la Senegal limeripoti kuwa boti iliyokuwa imebeba wahamiaji haramu imepinduka katika kaskazini mwa Senegal na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 23.

Ripoti imesema boti hiyo iliyokuwa imejaa wahamiaji haramu iliondoka tarehe 28 katika mji wa Sesimbur na kuelekea Hispania na kupinduka kaskazini mwa Hispania na kuzama karibu na mji wa bandari wa Saint-Louis nchini Hispania.

Idara ya zima moto ya Senegal imesema kulikuwa na takriban watu 280 ndani ya boti hiyo, na waokoaji wameokoa miili 23, na shughuli ya uokoaji bado inaendelea.