Watu 43 wafariki kutokana na moto mkubwa katika jengo la ghorofa nchini Bangladeshi
2024-03-01 08:51:19| CRI

Watu 43 wamefariki Alhamisi usiku baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo lenye ghorofa huko Dhaka, Bangladesh. Waziri wa Afya na Ustawi wa Familia wa Bangladesh Samanta Lah Sen amethibitisha vifo hivyo.

Waziri huyo amesema miili 33 imepelekwa katika Hospitali ya Chuo cha Matibabu cha Dhaka na mingine 10 katika Taasisi ya taifa ya Sheikh Hasina mjini Dhaka.

Ofisa wa Jeshi la Zimamoto amesema karibu watu 75 ikiwa ni pamoja na 42 waliokuwa kwenye hali ya kupoteza fahamu, waliokolewa kutoka kwenye moto na kukimbizwa hospitali, na kwamba waokoaji wanaendelea na kazi katika eneo hilo.

Ofisa mwingine wa zimamoto amesema idadi ya vifo katika ajali hiyo huenda itaongezeka.