Rais Xi asisitiza maendeleo ya hali ya juu ya nishati mpya nchini China
2024-03-01 23:37:05| cri

Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kwa dhati kuhimiza maendeleo ya hali ya juu ya nishati mpya nchini China ili kutoa mchango zaidi katika ujenzi wa dunia safi na nzuri.

Rais Xi aliyasema hivi karibuni akiongoza kikao cha utafiti cha kikundi cha Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na kubainisha kuwa usalama wa nishati unaathiri maendeleo ya jumla ya kiuchumi na kijamii ya nchi, na kuwa kuendeleza nishati safi na kuhimiza mabadiliko ya kijani na kaboni chache kumekuwa ni makubaliano ya jumuiya ya kimataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi duniani.

Maendeleo ya nishati ya China bado yanakabiliwa na mlolongo wa changamoto, kama vile shinikizo kubwa la mahitaji, vizuizi vya usambazaji, na kazi ngumu za mpito wa kijani na kaboni chache.

Rais Xi pia amesema kutokana na utajiri mkubwa wa nishati ya upepo, photovoltaic na rasilimali nyingine, China inaonyesha uwezo mkubwa wa maendeleo katika sekta ya nishati mpya.