UNECA yataka kufanyika kwa juhudi za pamoja kwa ajili ya maendeleo endelevu barani Afrika
2024-03-01 08:55:07| CRI

Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) imetoa wito kwa nchi za Afrika kufanya juhudi za pamoja ili kujenga uwezo wa kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi kwa uchumi wa Afrika.

Wito huo umetolewa na Bw. Antonio Pedro, naibu katibu mtendaji wa UNECA, ambaye amesema bara la Afrika linabeba mzigo mkubwa kutokana na kuwepo kwa hali ya sintofahamu duniani, huku dunia ikiingia kwenye hali tete ya kiuchumi, mabadiliko ya tabianchi, migogoro na kutoaminiana.

Bw. Pedro amesema bara la Afrika linahitaji kukumbatia mabadiliko ya muda mrefu ya kimuundo na uwekezaji wa kutosha, kwani changamoto inazokabiliana nazo Afrika kwa sasa ni kali, kwa sababu mfumo wa fedha duniani hautoshelezi na umeshindwa kabisa kuisaidia Afrika.