Rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi afariki dunia akiwa na umri wa miaka 98
2024-03-01 08:53:41| CRI

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa Rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia Alhamisi akiwa na umri wa miaka 98. Rais Samia ametangaza kifo hicho kupitia Shirika la Utangazaji la Tanzania, na kusema Rais Mwinyi amefariki dunia katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam saa kumi na moja na nusu jioni kutokana na saratani ya mapafu.

Rais Mwinyi alikuwa rais wa pili wa Tanzania akiwa madarakani kuanzia mwaka 1985 hadi 1995, akimrithi rais wa kwanza Julius Nyerere.

Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa kuanzia Ijumaa, ambapo bendera zote za taifa zitapeperushwa nusu mlingoti, na mazishi ya Rais Mwinyi yamepangwa kufanyika Machi 2.