Idadi ya vifo katika Ukanda wa Gaza yazidi 30,000
2024-03-01 08:51:19| cri

Tarehe 29 Februari ilikuwa siku ya 146 tangu kuanza kwa duru mpya ya mgogoro kati ya Palestina na Israel. Idara ya Afya ya Ukanda wa Gaza ilitoa taarifa siku hiyo na kusema idadi ya watu waliofariki kutokana na operesheni za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza imezidi 30,000.

Idara hiyo imesema katika taarifa yake kwamba licha ya zaidi ya watu 30,000 waliofariki, zaidi ya watu 70,000 wamejeruhiwa. Bado kuna idadi kubwa ya watu waliofukiwa chini ya vifusi, na timu ya uokoaji haiwezi kufika kwenye eneo la tukio.

Kwa mujibu wa taarifa nyingine iliyotolewa na idara hiyo, kituo cha kukusanyia vifaa vya msaada katika mji wa Gaza kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kilishambuliwa na jeshi la Israel mapema asubuhi ya siku hiyo. Watu 104 waliuawa na wengine 760 kujeruhiwa.