Teknolojia za kifedha za China zakaribishwa nchini Kenya
2024-03-01 08:52:54| CRI

Mwenyekiti wa Shirikisho la Teknolojia za Kifedha nchini Kenya (AFIK) Bw. Ali Hussein Kassim amesema kwenye ufunguzi wa Tamasha la kwanza la teknolojia za kifedha la Kenya kuwa kutokana na ongezeko la biashara kati ya Kenya na China, teknolojia za kifedha za China zinakaribishwa zaidi nchini Kenya.

Bw. Kassim amesema mifumo ya malipo ya China kama vile WeChat Pay na Alipay, inaweza kuzisaidia kampuni na watu binafsi wa Kenya kupunguza muda wa miamala ya kifedha wakati wa kufanya biashara na kampuni za China.

Ameongeza kuwa ni vizuri kutumia teknolojia za kifedha za China kwa sababu kuwa malipo yanahitaji dakika chache tu, na yana ufanisi zaidi kuliko ulipaji wa pesa wa jadi unaochukua siku mbili.