Mkutano wa pili wa awamu ya 14 ya kamati kuu ya CPPCC wafunguliwa kesho
2024-03-03 15:32:42| CRI


 

Mkutano na waandishi wa habari wa Mkutano wa pili wa awamu ya 14 ya Kamati kuu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC umefanyika leo, ambapo msemaji wa Mkutano wa mwaka huu Bw. Liu Jieyi amefahamisha hali husika ya mkutano huo na kujibu masuali ya vyombo vya habari vya nchini na nchi za nje.

 

Bw. Liu Jieyi amesema, Mkutano wa pili wa awamu ya 14 ya Kamati Kuu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China utafunguliwa kesho tarehe 4 Machi mchana katika Ukumbi wa mikutano ya umma wa Beijing, na kufungwa tarehe 10 Machi.