Watu 19 wauawa na mamba katika miaka mitano kwenye mwambao wa kusini mwa Tanzania wa Ziwa Victoria
2024-03-04 08:40:36| CRI

Takriban watu 19 waliuawa na mamba na wengine 20 kupoteza viungo vyao katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wilayani Sengerema mkoani Mwanza kwenye mwambao wa kusini mwa Tanzania wa Ziwa Victoria.

Afisa wanyamapori wa wilaya ya Sengerema, Paul Poncian, alisema watu 20 walipoteza viungo vyao baada ya kushambuliwa na mamba hao kati ya Januari 2019 na Disemba 2023, ambapo wengi wao ni wavuvi.

Aliwataja wahanga wengine kuwa ni waogeleaji na watu waliochota maji kwenye Ziwa Victoria, ambalo ni ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika na hifadhi kuu ya Mto Nile.

Ofisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Lolruck Mosses amesema mamlaka hiyo imeanzisha kampeni yenye lengo la kuwajengea uelewa wakazi wa karibu na ziwa hilo ili kuepuka mashambulizi ya mamba hao.