Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China laanza kikao cha mwaka leo
2024-03-04 08:53:38| CRI

Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambalo ni chombo kikuu cha ushauri wa kisiasa nchini China, litafanya kikao chake cha mwaka kuanzia leo tarehe 4 hadi tarehe 10 mwezi huu hapa Beijing.

Kikao cha pili cha Kamati Kuu ya 14 ya baraza hilo kitafunguliwa saa tisa leo alasiri na kufungwa asubuhi ya Machi 10.

Msemaji wa kikao hicho Liu Jieyi amesema, katika mwaka uliopita, washauri wa kisiasa wamezingatia zaidi kutoa ushauri wa ujenzi wa China kuelekea kuwa nchi ya kisasa. Jumla ya shughuli 94 za mashauriano zilifanyika mwaka huu, ambazo zilihusu mada mbalimbali, ikiwemo kuanzishwa kwa mtindo mpya wa maendeleo, huku shughuli 138 za utafiti na uchunguzi zikiwa zimefanywa na washauri wa kisiasa.