Afrika inaihitaji China kwa maendeleo ya kidijitali
2024-03-04 14:23:00| cri

Nchi za Afrika zimetajwa kuwa zinaihitaji China kwa ajili ya maendeleo ya teknolojia za kidijitali zenye faida na zinazowezekana kwa watu katika nchi za Kiafrika. Teknolojia hizo zimetajwa kuwa ni pamoja na zile za huduma za afya, kukuza upatikanaji wa elimu na kujifunza mambo ya maisha, na kuongeza ushirikishwaji wa kifedha.

Hata hivyo nchi za Afrika zinakosa miundombinu ya kimsingi inayohitajika kuunganisha jamii kwa teknolojia hizo.

Mwaka wa 2023 ni asilimia 83 tu ya wakazi wa Afrika Kusini mwa Sahara waliohudumiwa na angalau mtandao wa simu wa 3G. Katika maeneo mengine duniani huduma ilikuwa zaidi ya asilimia 95. Katika mwaka huo huo, chini ya nusu ya idadi ya watu barani Afrika walikuwa na huduma ya mtandao wa simu, wakiwa nyuma ya nchi za Kiarabu (asilimia 75) na eneo la Asia-Pasifiki (asilimia 88).