Mkutano wa pili wa awamu ya 14 ya Kamati kuu ya CPPCC wafunguliwa
2024-03-04 15:41:25| cri

Mkutano wa pili wa awamu ya 14 ya Kamati kuu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) umefunguliwa leo saa tisa alasiri katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing. Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Rais wa China, na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya Chama Xi Jinping pamoja na viongozi wengine wa Chama na serikali wamehudhuria ufunguzi wa mkutano huo.

Muhula wa wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China ni miaka mitano, na mkutano wa wajumbe wote wa Baraza hilo hufanyika kila mwaka. Katika mkutano huo, wajumbe watajadili mambo ya kisiasa, na kutoa busara kwa ajili ya maendeleo ya kitaifa yenye sifa ya juu.