Algeria na Iran zasaini makubaliano mbalimbali ya ushirikiano
2024-03-04 08:52:57| CRI

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune jana Jumapili amesaini makubaliano mbalimbali ya ushirikiano na mwenzake wa Iran Ebrahim Raisi ambaye yupo kwenye ziara ya kiserikali nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la APS, makubaliano hayo yanahusisha sekta za nishati, uanzishaji wa biashara, utalii na habari na mawasiliano.

Rais Tebboune ameeleza nia yake ya kuhimiza ushirikiano kati ya Algeria na Iran akiuelezea uhusiano wao kuwa wa “kihistoria”. Pia ameipongeza Iran kwa kuiunga mkono Algeria katika uwanachama usio wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuonesha mshikamano wake kwa watu wa Palestina.

Kwa upande wa Raisi, pia amesisitiza kuimarisha uhusiano na Algeria na kutaka kupanua ushirikiano wao wa kiuchumi.