Makumi ya wapalestina wauawa au kujeruhiwa katika shambulizi la Israel katika mji wa Gaza
2024-03-04 09:07:53| CRI

Msemaji wa wizara ya afya ya kundi la Hamas Bw. Ashraf al-Qedra jana alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa makumi ya wapalestina waliuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulizi la Israel walipokuwa wakisubiri msaada katika mji wa Gaza.

Habari zilisema kwamba vikosi vya Israel viliwafyatulia risasi watu katika roundabout ya Kuwait, kusini mwa Mji wa Gaza, walipokuwa wakisubiri malori ya misaada yaliyobeba unga.

Kwa mujibu wa televisheni ya serikali ya Palestina, mapema Jumapili ndege za kivita za Israel zililishambulia kwa mabomu lori dogo lililokuwa na misaada ya kibinadamu huko Deir al-Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wanane.

Hadi sasa Israeli haijasema chochote kuhusu matukio hayo.