Rwanda yachukua hatua kusimamia biashara ya fedha mtandaoni
2024-03-04 14:20:32| cri

Biashara ya ubadilishanaji wa fedha za kigeni mtandaoni nchini Rwanda, kwa mara ya kwanza inasimamiwa baada ya kanuni husika kutolewa na serikali.

Kanuni za Februari 26, kanuni zinazosimamia biashara ya ubadilishanaji wa fedha za kigeni nchini Rwanda zilichapishwa katika Gazeti Rasmi la Februari 27, na kutolewa na Mamlaka ya Soko la Mitaji la Rwanda (CMA Rwanda).

Kwenye taarifa yake kwa umma kuhusu kanuni hizo ya Machi 1, mamlaka ya soko hilo inaona kuwa kanuni hizo zinaambatana na mamlaka yake ya kuwezesha maendeleo ya soko, huku ikihimiza ulinzi wa wawekezaji katika soko la mitaji la Rwanda.

Biashara ya ubadilishanaji wa fedha za kigeni yenye manufaa, imetajwa kuwa ni biashara ya inayofanywa mtandaoni kuwezesha wafanyabiashara kufanya biashara kwa kubadilishana safaru.