Mkuu wa Jeshi la Sudan ataka Sudan irejeshewe uanachama katika Umoja wa Afrika
2024-03-04 09:01:51| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Mamlaka ya Mpito la Sudan Bw. Abdel Fattah Al-Burhan amesisitiza imani ya Sudan kwa Umoja wa Afrika, huku akitoa mwito wa kurejesha uanachama kamili wa Sudan katika jumuiya ya kikanda.

Al-Burhan amesema hayo wakati akipokea ujumbe wa Jopo la ngazi ya juu la Umoja wa Afrika kuhusu utatuzi wa mgogoro nchini Sudan, ulioongozwa na Mohamed Ibn Chambas katika Bandari ya Sudan, mji mkuu wa jimbo la bahari ya Sham.

Baraza hilo limetoa taarifa ikisema, Al-Burhan ameeleza imani ya Sudan kwa Umoja wa Afrika na utatuzi uliotolewa nao, ikiwa nchi hiyo inachukuliwa na jumuiya hiyo kama mwanachama kamili.

Al-Burhan amesisitiza zaidi kuwa msingi wa suluhisho liko katika kuondolewa kwa kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kwenye miji na vijiji vilivyokaliwa na kikosi hicho.