Waziri mkuu wa China azungumzia kazi ya diplomasia katika ripoti ya kazi ya serikali
2024-03-05 12:28:37| cri

Waziri mkuu wa China Li Qiang ameeleza katika ripoti ya kazi ya serikali kuwa, China inatakiwa kushikilia sera ya kidiplomasia ya amani ya kujiamulia mambo na njia ya kujiendeleza kwa amani, kufuata kithabiti mkakati wa kufungua mlango wa kunufaishana, kuhimiza dunia yenye ncha nyingi ambayo ina usawa na utaratibu, na mafungamano jumuishi ya kiuchumi duniani, kusukuma mbele ujenzi wa uhusiano mpya wa kimataifa, kupinga umwamba, na kulinda haki na usawa wa kimataifa. Pia amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, kutekeleza Pendekezo la Maendeleo Duniani, Pendekezo la Usalama Duniani na Pendekezo la Ustaarabu Duniani, ili kuenzi thamani ya pamoja ya binadamu wote, kuhimiza mageuzi ya utaratibu wa usimamizi wa dunia, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.