Maafisa wa Afrika wakutana mjini Nairobi kujadili biashara haramu ya silaha
2024-03-05 09:12:01| CRI

Wajumbe kutoka nchi 26 za Afrika wanahudhuria mkutano wa nne wa kupitia mpango wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia, kupambana na kutokomeza biashara ya silaha ndogo na nyepesi huko Nairobi nchini Kenya wakisema kuwa nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara zimeazimia kuzuia biashara za silaha ndogo na nyepesi kutokana na kuleta tishio kwenye amani, utulivu na ukuaji wa muda mrefu.

Maafisa waliohudhuria mkutano huo walilaani uvushaji wa silaha hizi mipakani, kuchochea ugaidi, uasi wa kutumia silaha na uhalifu wa wanyamapori.

Katibu mkuu wa wizara ya usalama wa ndani na utawala wa kitaifa wa Kenya Bw. Raymond Omollo alisema kuwa kuenea kwa matumizi mabaya ya silaha ndogo na nyepesi kunatishia amani, mshikamano na utulivu wa Afrika.