Somalia yakamilisha mchakato wa kujiunga na EAC
2024-03-05 08:55:32| CRI

Somolia jana Jumatatu iliwasilisha hati ya idhini ya Mkataba wa Kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa katibu mkuu wa jumuiya hiyo katika makao makuu yake mjini Arusha, Tanzania, na kuifanya nchi hiyo kuwa mwanachama rasmi wa nane wa jumuiya hiyo ya kikanda.

Taarifa iliyotolewa Jumatatu na makao makuu ya EAC inasema kulingana na itifaki za kupokea wanachama wapya, Katibu Mkuu wa EAC Peter Mathuki ameitangaza Somalia kuwa mwanachama mpya wa jumuiya hiyo.

Wanachama wengine saba wa EAC ni Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda na Tanzania.