China yatimiza malengo makuu ya mwaka 2023
2024-03-05 10:27:11| cri

China imetimiza malengo na majukumu yake makuu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya mwaka 2023, licha ya matatizo na changamoto nyingi kutoka ndani na nje ya nchi.

Ripoti ya kazi ya serikali iliyowasilishwa Jumanne kwa bunge la umma kwa ajili ya kujadiliwa, imesema katika kipindi hicho pato la taifa la China liliongezeka kwa asilimia 5.2, na kuwa moja ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi duniani.

Katika mwaka huo nafasi za ajira milioni 12.44 ziliundwa mijini, na wastani wa kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kilikuwa asilimia 5.2. Fahirisi ya bei ya walaji iliongezeka kwa asilimia 0.2, na usawa wa kimsingi ulidumishwa katika uwiano la malipo.