China inalenga ukuaji wa uchumi wa karibu asilimia 5 kwa mwaka huu
2024-03-05 10:28:50| cri

Ripoti ya kazi ya serikali iliyowasilishwa Jumanne kwenye bunge la umma la China kwa ajili ya kujadiliwa, inasema China inalenga ukuaji wa uchumi wa karibu asilimia 5 kwa mwaka huu.

China inatarajia kuunda zaidi ya nafasi milioni 12 za ajira katika maeneo ya mijini na kuweka kiwango cha ukosefu wa ajira mijini katika karibu asilimia 5.5.

Sera za fedha zitaendelea, huku uwiano wa nakisi kwa pato la taifa (GDP) ukiwekwa kuwa asilimia 3 na nakisi ya serikali itaongezeka kwa yuan bilioni 180 ikilinganishwa na takwimu za bajeti ya 2023. Imefahamika pia kutakuwa na Yuan trilioni 3.9 za dhamana za maalum kwa serikali za mitaa, zikiwa zimeongezeka kwa Yuan bilioni 100 ikilinganishwa na mwaka jana.

Serikali pia itatoa hati fungani za muda mrefu zaidi katika kila miaka kadhaa ijayo kwa madhumuni ya kutekeleza mikakati mikuu ya kitaifa, na kujenga uwezo wa kiusalama katika maeneo muhimu, kuanzia na hati fungani yenye thamani ya Yuan trilioni 1 mwaka huu.

Ripoti pia imesema uthabiti wa mwelekeo wa sera ya jumla unapaswa kuimarishwa.