Kenya Jumatatu ilizindua mradi wa kuimarisha usalama wa nchi hiyo kwa kuratibu usimamizi mipakani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa Bw. Raymond Omollo amesema kuwa mradi huo ni hatua muhimu ya kuhakikisha usalama na ufanisi kwenye bandari za kuingia na kutoka, ambao unahusisha muundo wa usimamizi kwa ajili ya ushirikiano na mwelekeo na teknolojia zinazoibuka, na pia unajumuisha uratibu wa ndani na kati ya mashirika ya nchi hiyo, pamoja na uratibu wa kimataifa unaohusisha ushirikiano kati ya nchi jirani na washirika wa kibiashara.
Kwa mujibu wa Bw. Omollo, kupitia mradi huo, Kenya itakuwa na njia inayoratibiwa na inayofaa zaidi ya kukabiliana na uhalifu wa kupangwa na matishio mengine yanayodhoofisha amani, usalama na maendeleo endelevu.