Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China wafunguliwa
2024-03-05 10:52:20| cri

Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China umefunguliwa leo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma wa Beijing, na kuhudhuriwa na karibu wajumbe 3,000 kutoka sehemu mbalimbali, makabila mbalimbali na sekta mbalimbali.

Bunge la Umma ni mamlaka ya juu zaidi ya China, na muhula wa wajumbe ni miaka 5. Bunge hilo huitisha mkutano wa wajumbe wote kila mwaka, ili kujadili na kuamua mambo muhimu mbalimbali, ikiwemo sera, sheria na uteuzi wa maafisa muhimu. Mkutano wa mwaka huu utapitia ripoti ya kwanza ya kazi iliyotolewa na awamu mpya ya serikali, hivyo unafuatiliwa na watu kutoka sekta mbalimbali.