China na Algeria zatarajia kuzidisha ushirikiano wa kiuchumi
2024-03-06 09:18:58| CRI

Maofisa waandamizi na wajumbe wa kibiashara kutoka China na Algeria wamekusanyika huko Setif, mashariki mwa Algeria kuhudhuria mkutano wa baraza la uchumi kati ya China na Algeria.

Mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na ubalozi wa China nchini Algeria na serikali ya mkoa wa Setif, umehudhuriwa na washiriki 260 wakiwemo wabunge na maofisa wa serikali wa Algeria pamoja na wadau wa biashara kutoka nchi zote mbili.

Balozi wa China nchini Algeria Bw. Li Jian ametoa hotuba katika mkutano huo akisema, uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Algeria umeingia katika kipindi kipya, na ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara umepiga hatua kubwa, wakati thamani ya biashara ya mwaka kati ya pande mbili ikizidi dola bilioni 10 kwa mara ya kwanza katika mwaka 2023.

Bw. Li amesema, anatumai mkoa wa Setif, wenye uwezo mkubwa katika kilimo, maliasili za madini, ukuaji wa viwanda, utalii na utamaduni, utaweza kuwa mlango wa ushirikiano kati ya China na Algeria.