Viongozi wa China wahudhuria mijadala katika kikao cha kila mwaka cha bunge
2024-03-06 08:54:36| CRI

Viongozi mbalimbali waandamizi wa China Jumanne walihudhuria mijadala kwenye kikao cha pili cha Bunge la 14 la Umma la China (NPC).

Alipojiunga na mjadala wa kikundi na manaibu wa bunge kutoka Mkoa wa Yunnan, Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, alisisitiza kwamba Yunnan inapaswa kuonesha kikamilifu faida na sifa zake ili kuunganishwa vyema katika mkakati wa kitaifa wa maendeleo yaliyoratibiwa ya mikoa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma Zhao Leji, alipojiunga kwenye mjadala na wajumbe wenzake kutoka mkoa wa Sichuan, alitaka mkoa huo kutekeleza maamuzi na mipango iliyotolewa na Kamati Kuu ya CPC kwa kuzingatia hali yake halisi, na kusukuma mbele ujenzi wa China ya kisasa.

Naye mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Wang Huning, aliungana na manaibu kutoka Mkoa wa Guizhou katika majadiliano, akitoa wito kwa mkoa huo kuendeleza ufufuaji wa vijijini kwa pande zote na kuimarisha na kupanua mafanikio katika kupunguza umaskini.

Ding Xuexiang, naibu waziri mkuu wa China, aliungana na wabunge wenzake kutoka Mkoa wa Kaskazini mashariki wa Liaoning kujadili ripoti ya kazi ya serikali, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kwa karibu kazi kuu ya Chama katika zama mpya na safari mpya na kukuza maendeleo yenye ubora wa juu ili kupata matokeo thabiti.

Akiungana na wabunge wenzake wa Jimbo la Fujian kujadili ripoti ya kazi ya serikali, afisa mkuu wa China anayepambana na ufisadi Li Xi alisisitiza juhudi za kuboresha zaidi ukaguzi na usimamizi wa nidhamu wa hali ya juu, ili kutoa uhakikisho thabiti wa kuijenga China kuwa nchi kubwa na kutimiza ustawi mpya wa taifa.