China yaiomba jumuiya ya kimataifa kusaidia kuhimiza mchakato wa kisiasa nchini Sudan Kusini
2024-03-06 09:04:07| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing jana alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia kuhimiza mchakato wa kisiasa nchini Sudan Kusini na kuunga mkono nchi hiyo kuimarisha ujenzi wa uwezo katika sekta ya usalama.

Balozi Dai alisema kuwa mwaka huu una umuhimu mkubwa kwa Sudan Kusini katika suala la kuhimiza mpito wa kisiasa na maendeleo ya amani. China inaamini kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza uungaji mkono wake kwa Sudan Kusini.

China inaunga mkono pande za Sudan Kusini katika kuharakisha utekelezaji wa makubaliano ya amani na vigezo muhimu vya mwongozo wa kuongeza muda wa mpito, ili kuweka mazingira yanayofaa kwa mpito wa kisiasa na kufanyika kwa uchaguzi mkuu. China inahimiza utaratibu wa pande tatu wa Umoja wa Afrika, Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo (IGAD), na Umoja wa Mataifa kuunga mkono zaidi kwenye mchakato wa kisiasa nchini Sudan Kusini.