Ethiopia yazindua huduma ya kibunifu ya data ya satelaiti kwa ushirikiano na China
2024-03-06 23:03:43| cri

Mkurugenzi wa Operesheni za satelaiti wa Taasisi ya Sayansi ya Anga ya juu na taasisi ya mambo ya ardhi ya Ethiopia (SSGI) Bwana Melaku Muka amesema taasisi hizo zimezindua mpango wa "kituo cha ardhini ", unaohusisha upokeaji wa data za satelaiti kwa ajili ya nchi hiyo.

Bwana Melaku amesema taasisi hizo zimeanza kupata mapato kwa kupokea data za satelaiti, kuzitayarisha na kuzichambua kwa mashirika na nchi mbalimbali kwa msingi wa malipo. Kituo cha ardhini kilichojengwa na kampuni ya China kwenye Kituo cha Utafiti wa Sayansi ya Anga cha Entoto huko Addis Ababa, ni sehemu muhimu ya mpango huu, kikiwa na uwezo wa kupokea data za satellite zenye ubora wa juu.