Rais Xi Jinping wa China jana alasiri aliposhiriki kwenye mjadala wa ujumbe wa mkoa wa Jiangsu kando ya kikao cha pili cha Bunge la 14 la umma la China, amesisitiza kuendeleza tija mpya yenye ubora kulingana na hali halisi ya maeneo tofauti, na kushikilia jukumu la kipaumbele la kutimiza maendeleo yenye ubora wa juu.
Rais Xi amesema wakati dunia inashuhudia duru mpya ya mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia na mageuzi ya kisekta, China inatakiwa kutumia vyema fursa, kuongeza nguvu katika kufanya uvumbuzi, kukuza sekta mpya zinazoibuka, kupangilia na kujenga sekta za siku zijazo, ili kukamilisha mfumo wa viwanda vya kisasa.