Kenya yalitaka bunge la Afrika Mashariki kuongeza juhudi za kukuza mafungamano
2024-03-06 08:55:14| CRI

Rais wa Kenya William Ruto Jumanne alilitaka Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kuimarisha juhudi za mafungamano ya kikanda, na kuiweka Afrika Mashariki kama mfano wa kuigwa katika bara hilo.

Akiongea kwenye ufunguzi rasmi wa mkutano wa tatu wa kikao cha pili cha bunge la tano la EALA mjini Nairobi, nchini Kenya, Ruto pia alibainisha kuwa EALA, na mabunge mengine ya kikanda, yanafaa pia kutekeleza jukumu lao katika kulifanya Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika liwe kitovu kinachofuata cha uwekezaji wa kimataifa, biashara na viwanda. Amesisitiza kuwa ili kufikia hili, inabidi wakamilishe utekelezaji wa nguzo zote za mafungamano ya EAC na kuoanisha kwa kina ajenda yao ya mafungamano na dhana pana ya mabadiliko ya Afrika chini ya Afrika Wanayoitaka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais, Ruto alisema bara la Afrika ni tajiri na linahitaji tu mali yake kuthaminiwa ipasavyo, akibainisha kuwa hivi karibuni Afrika itakuwa soko kubwa zaidi duniani.