Kenya yazindua kampeni ya kukuza utalii wa ndani
2024-03-06 09:18:23| CRI

Bodi ya utalii ya Kenya KTB jana Jumanne ilizindua kampeni ya kuhimiza utalii wa ndani.

Kaimu afisa mtendaji mkuu wa KTB Bw. John Chirchir amesema huko Nairobi kwamba mpango huo wa mwezi mzima ni pamoja na kuwatuza wenyeji wanaotembelea vivutio vya utalii kote nchini.

Bw. Chirchir amesema, kampeni hiyo ni kiashirio cha hamu inayoongezeka kati ya wakenya wanaotaka kugundua tena nchi yao kwa kujionea mvuto wa lulu zilizofichwa kupitia upande mpya.

Takwimu kutoka Shirika la Viwango la Kenya zimeonesha kuwa sekta ya utalii ni moja kati ya vyanzo vikuu vya fedha za kigeni, pamoja na mauzo ya bidhaa za kilimo cha bustani na chai kwa nje na utumaji wa fedha kutoka kwa diaspora.