Mabaharia wawili wauawa kwenye shambulizi la kundi la Houthi la Yemen dhidi ya meli ya mizigo
2024-03-07 09:01:34| CRI

Mabaharia wawili wameuawa, watatu kujeruhiwa na wengine watatu wakiwa hawajulikani walipo katika shambulizi la makombora lililofanywa na kundi la Houthi la Yemen dhidi ya meli moja ya kibiashara iliyodaiwa ni ya Marekani wakati ikivuka Ghuba ya Aden.

Vyanzo vya habari kutoka kwa Walinzi wa Pwani ya Yemen vimeliambia Shirika la Habari la Xinhua kwamba meli hiyo iitwayo“True Confidence” ilishambuliwa na makombora kadhaa katika umbali wa maili 50 za baharini kusini magharibi mwa bandari ya Aden, na mabaharia wengi wa meli hiyo walifanikiwa kuondoka melini kwa boti za kuokoa maisha wakati meli ilipokaribia kuzama, ila sasa watatu bado hawajulikani walipo.