Viongozi EAC kumuunga mkono Raila Odinga kugombea uenyekiti Kamisheni ya Umoja wa Afrika AUC
2024-03-07 23:33:14| cri

Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameahidi kumuunga mkono mgombea mmoja wa uenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC). Hayo yametangazwa mjini Nairobi na Rais wa Kenya, William Ruto alipohutubia Bunge la Afrika Mashariki (EALA).