Zaidi ya asilimia 80 ya waliohojiwa duniani wasifu sera ya kidiplomasia ya China
2024-03-07 20:45:56| CRI

Hivi karibuni hojaji iliyoandaliwa kwa pamoja na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na Chuo Kikuu cha Umma cha China na kufanyika kwa kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mawasiliano ya Kimataifa ya Zama Mpya imeonesha kuwa, asilimia 83.5 ya waliohojiwa wanasifu sera ya kidiplomasia ya amani ya China ambayo inajiamulia mambo, wakiamini kuwa hii itasaidia ujenzi wa utaratibu wa kimataifa wenye haki zaidi.

Hojaji hiyo inahusisha waliohojiwa 31,980 kote duniani ikiwa ni pamoja na nchi zilizoendelea zikiwemo Marekani, Ujerumani, Ufaransa na Japan, na nchi zinazoendelea kama vile Mexico, Thailand na Nigeria.