Wang Yi: jumuiya ya kimataifa lazima ichukulie usitishaji mapigano mara moja na kukomesha vita kama kipaumbele
2024-03-07 11:34:16| cri

Kwenye Mkutano na waandishi wa habari kando ya Mkutano wa pili wa Bunge la 14 la Umma la China, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema jumuiya ya kimataifa lazima ichukulie usitishaji wa mapigano mara moja na kukomesha vita kama kipaumbele chake kikuu, na watu wa Gaza wana haki ya kuishi. Amesema China inaunga mkono Palestina kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa.