Rais Xi Jinping wa China jana alasiri aliwatembelea wajumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) kutoka kamati ya kimapinduzi ya Koumintang ya China, sekta ya sayansi na teknolojia na sekta ya raslimali za mazingira, ambapo alishiriki kwenye mjadala wao na kusikiliza maoni na mapendekezo yao.
Rais Xi amesisitiza kuwa wajumbe wa CPPCC kutoka vyama mbalimbali, makundi mbalimbali, makabila mbalimbali na sekta mbalimbali wanapaswa kufanya uchunguzi wa kina, kujituma katika kutoa mashauri na mapendekezo, na kukusanya maafikiano mapana chini ya majukumu ya kimkakati yaliyotajwa kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mipango iliyowekwa kwenye mkutano wa kazi za uchumi wa kamati kuu ya CPC, ili kuchangia juhudi za kuijenga China kuwa nchi ya kisasa.